Jina langu ni RODGERS HEMEDI GUMBO Mkurugenzi wa TWIN FREIGHT FORWARDERS LTD.
Nina elimu ya SHAHADA YA KWANZA YA BIASHARA NA UCHUMI kutoka CHUO KIKUU CHA HONG KONG. Nina UZOEFU wa Kazi na Uongozi kutoka taasisi zifuatazo:
1. Wizara ya VIWANDA na BIASHARA (SADC Department)
2. BOT -Benki Kuu ya Tanzania
3.YANGA -Young Africans Sports Club- MJUMBE wa Kamati Tendaji Na MWENYEKITI Kamati Ya Mashindano.
Nawashukuru kwa kuniamini kunichagua kwenye uongozi awamu iliyopita. Tumefanya kazi kubwa:
- Kuboresha mifumo ya ndani ya utendaji wa chama
- Kurekebisha na kuimarisha utaratibu na mawasiliano ya TAFFA makao makuu na ofisi za mipakani baada ya kuzitembelea zote
- Kukuza mahusiano na wadau wetu muhimu ambayo ilikuwa imeharibika
- Tumesimamia uanzishaji container guarantee na kanuni zake
Tuliyofanya ni msingi wa mazuri yanayokuja. NAOMBA KURA YENU YA NDIO ili niweze kutekeleza:
- Kuboresha usimamizi wa fedha za wanachama
- Mazingira mazuri kwa wafanyakazi wa kampuni wanachama
- Ufuatiliaji wa utendaji wa bandari kavu
- Kuongeza huduma za guarantee ya makontena na kupunguza bei.