Kwa majina Ninaitwa Ebenezer Kwayu, ni Mgombea Ujumbe TAFFA 2023. Ninayo Elimu ya Degree ya Kwanza Kutoka Chuo Kikuu Mzumbe katika Maswala ya Uhasibu na Fedha. Ninayo Elimu ya Cheti cha Ujasiriamali Kutoka Chuo Kikuu Cha Bocconi (Millano - Italy)
Pia Ninayo Elimu ya Africa Mashariki Katika Kodi ya Forodha na Uondoshaji wa Mizigo Bandarini Kutoka Chuo Cha Kodi Tanzania (ITA). Ninao Utashi wa Kuleta Mabadiliko Nikishirikiana na Wakurugenzi na Wadau Mbalimbali Katika Tasnia Yetu. Nina uwezo wa Kuhasi Mifumo Kandamizi na Kusimamia Maslahi ya Tasnia.
Nimefanya Kazi Katika Mazingira Ambayo Mengine siyo Rafiki, hivyo nimeona ni busara Kuiomba nafasi hii Ili niweze Kushirikiana na Wenzangu Kwa Vitendo Kuondoa Changamoto Hizi lengo likiwa ni Kuboresha Mazingira Yetu Ya Kazi. Ninaamini Kila Jambo Linawezekana. Na Zaidi Tukimtegemea Mwenyenzi Mungu Yote Nitakayoyafanya Yatafanyika Kuwa Baraka Kwa Kila Mmoja Atakayenichagua Kuwa Kiongozi Wake. Hutapoteza Kura Yako!